Sheria mpya ya uraia yaleta vurugu India

Your browser doesn’t support HTML5

Polisi nchini India imewakamata darzeni za watu wanaopinga sheria mpya ya uraia wakati wa maandamano Alhamisi, Disemba 18, 2019.
Maandamano hayo yanaonyesha upinzani wa hali ya juu ambao Waziri Mkuu Narendra Modi amewahi kukabiliwa nao tangu alipochukuwa madaraka miaka sita iliyopita ambapo alikuwa anafaidika na wimbi la kukubalika.
Serikali ya Modi ina nguvu ikiwa ni ya waliowengi katika chama chake na wachache katika serikali yake walitegemea machafuko dhidi ya sheria hiyo iliyopitishwa.