Duniani Leo June 13th, 2019

Your browser doesn’t support HTML5

Ndani ya Duniani Leo: Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vingine mashariki ya kati ikiwa jumuia ya kimataifa haitokuwa na ustahmilivu wa kutafuta njia za kupunguza mvutano kati ya Marekani na Iran. Abe yuko Iran kwa ziara ya siku tatu katika lengo la kutafuta suluhisho la kidiplomasia la kupunguza uhasama kati ya mataifa hayo mawili, uhasama ambao unazusha wasi wasi wa kutokea mzozo mwengine katika kanda ya mashariki ya kati.