Kenya Airways yaanza kuwapunguza wafanyakazi

Mbuvi Nguzi Mkurugenzi mkuu wa KQ akikaribisha ndege ya pili ya 787 Dreamliner

Shirika la nedge ya Kenya, limeanza kuiwaachisha kazi wafanyakazi wake katika mpango wa kufanya marekebisho ya matumizi na kuongeza mapato.

Mbuvi Ngunze Mkurugenzi Mtendaji wa Kenya Airways

Kulingana na mpango huo hadi watumishi 600 wanatazamiwa kuachishwa kazi katika muida huu ambao Kenya Airways inapata hasara kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wake Mbuvi Nguze.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Mkuregenzi wa Kenya Airways Mbuvi Ngunze

Akizungumza na Sauti ya Amerika Bw. Ngunze amesema mpango huo utafanyika katika awamu tatu tofauti ambapo wiki hii watu 80 waliaachishwa kazi. "Uwamuzi huu ulichukuliwa hapo mwezi March 2016 kwa sababu tulisema tumepunguza zile ndege tulizonazo na pia tutatafuta njia za kuimarisha mapato na hivyo tutapunguza wafanyakazi".

Chama cha wafanyakazi cha marubani kililalamika na kuwataka wanachama wake kugoma hapo mwezi March pale mpango ulipotangazwa na kumlazimisha mkurugenzi wa watumishi wa shirika hilo Alban Mwendar kuondolewa.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka minne ambapo shirika hilo maarufu ya Afrika inawapunguza wafanyakazi wake katika kupunguza matumizi na kuongeza faida.