Kesi ya kupinga ushindi wa rais Museveni imeanza kusikilizwa

Amama Mbabazi, mgombea wa vugu vugu la Go Forward akizungumza na waandishi wa habari.

Kesi ya kupinga ushindi wa rais Museveni wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa Uganda uliofanyika mwezi Februari, imeanza kusikilizwa Jumatatu katika mahakama kuu nchini humo.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Kennes Bwire

Huku mawakili wakikosa kukubaliana jinsi ya kuendesha kesi hiyo, siku nzima
mawakili wake aliyekuwa mgombea wa urais Amama Mbabazi walifanyia mabadiliko ya orodha ya mambo mahakama hiyo inafaa kushughulikia, wakitaka hesabu ya kura katika wilaya 42 kurudiwa, jambo ambalo mawakili wa rais Museveni na wale wa tume ya uchaguzi walipinga.
Vikao vya mahakama viliahirishwa mara kadhaa, lakini hatimaye jopo la majaji tisa, wakakubali ombi la Amama Mbabazi.