Aboud: Mazungumzo Yanaendelea juu ya Uchaguzi Zanzibar

Mashabiki wa chama cha CUF waandamana mjini Unguja, Zanzibar

Kufutwa kwa uchaguzi wa rais katika visiwa vya Zanzibar ni suala ambalo bado linaendelea kuleta utata nchini Tanzania, huku upande wa chama cha upinzani CUF ukisisitiza kwamba uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na upande wa chama tawala CCM ukiunga mkono kauli ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa visiwa hivyo Salum Jecha akitaka uchaguzi huo urudiwe.

Mohamed Aboud,Waziri wa Nchi katika Afisi ya Makamu wa pili wa Rais

“Mimi si mshiriki wa mazungumzo sina taarifa ya mazungumzo hayo” alisema waziri wa nchi ofisi ya makamu rais wa Zanzibar Mohamed Aboud alipozungumza na VOA Jumanne.

Akizungumzia suala la wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya Bunge la taifa huko Dodoma, Bw, Aboud alisema kwamba wale waliochaguliwa watakwenda kwani uchaguzi wa Muungano haujaharibika, bali ule wa Zanzibar ndio ulikua na hitilafu.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Mohamed Aboud

Bw. Aboud alishauri watu kusubiri hadi pale suluhishop litapatikana kutokana na mazungumzo yanayoendelea, na kwamba kwa wakati huu serikali ya Zanzibar inaendelea na kazi zake za kawaida.