Kampeni zaanza rasmi nchini Uganda.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu nchini Uganda zimeanza rasmi hii Jumatatu, wanaowania urais wakivutia umati mkubwa wa wapiga kura. Rais wa sasa Yoweri Museveni amekuwa wilayani Luweero, eneo lililoshuhudia vita vikali wakati alipoingia madarakani kwa kuipindua serikali iliyokuwepo mamlakani kwa wakati huo, akiendeleza ujumbe wa kuwataka wapiga kura kutowaamini wapinzani wake.

Dkt. Kiiza Besigye wa FDC naye amevutia umati mkubwa katika wilaya ya Rukungiri, alikozaliwa akihubiri siasa za kumng’oa Museveni madarakani huku Amama Mbabazi akiwa wilayani Masaka na ujumbe huo huo wa mageuzi.

Your browser doesn’t support HTML5

Kampeni Uganda zaanza rasmi.2"18'

Wakati huo huo Uganda imetuma wanajeshi 600 nchini Somalia kwa vita dhidi ya wanamgambo wa Al-shabaab. Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenerali Katumba Wamala amesisitiza kwamba ni lazima Uganda itatimiza lengo ililoanza mwaka 2007, la kuifanya Somalia kuwa nchi salama, akihimiza nchi za Afrika mashariki kuimarisha juhudi za pamoja kuangamiza kundi hilo kwa kuzingatia kwamba Al-shabaab ni maadui wa jumuiya ya Afrika mashariki na wala sio Somalia.

Your browser doesn’t support HTML5

Uganda yapeleka wanajeshi Somalia.2".25'