Wanafunzi Kurudi Mashuleni Nepal

Maelfu ya watoto nchini Nepal, walioathirika na tetemeko la ardhi wamerejea mashuleni ikiwa ni wiki tano baada ya tetemeko lililochukuwa maisha ya watu 8,600.

Watoto walipita kwenye vifusi na mabaki kuelekea katika madarasa ambayo yemefunguliwa kwenye mahema na madarasa ya dharura yaliyojengwa kwa kutumia plastiki.

Maafisa wa polisi wamesema wanafunzi watashauriwa kuzungumzia tetemeko hilo kwa waalimu ambao wamepitia mafunzo ya kuwasaidia wanafunzi kuondokana na msongo kufuatia tukio hilo.

Inaelezwa kwamba masomo rasmi yanatarajiwa kuanza wiki mbili zijazo.