Mpango wa amani wa Nyuklia wa Marekani na Iran unakwenda vyema

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, na Iran, Javad Zarif.

Mkuu wa masula ya nyuklia wa Iran, anasema maafisa wa Iran, wamefikia maelewano pamoja na wenzao wa Marekani, na washirika wanaojadiliana katika masuala mengi, lakini White House, haikupatia umuhimu matumaini hayo.

Bwana Ali Akbar Salehi, ameiambia televisheni ya serikali ya Iran, kwamba tofauti moja muhimu imebaki na maafisa watajaribu kufikia muafaka, japokuwa hakuweka wazi tofaiti yenyewe.

Amesema kama ikifanikiwa pande zote mbili zitakubaliana katika mambo ya kiufundi yanayojadiliwa Uswisi.

Msemaji wa White house, Josh Ernest, Jumanne amesema pande zote mbili zilifikia maendeleo muhimu mwaka uliopita lakini kuna asilimia 50 ya kuelekea kufikia muafaka.