Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anaendelea vizuri katika hopital maarufu ya John Hopkins mjini Baltimore, jimbo la Maryland baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume-prostate.
Kufuatana na maafisa walofuatana na Rais Kikwete hapa Marekani ni kwamba madaktari walomfanyia uchunguzi walipendekeza afanyiwe upasuaji huo ulofanyika bila ya matatizo.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Katibu wa Rais wa Tanzania Prosper Mbena amesema "hali ya rais inaendelea vizuri na hatuwezi kujuwa atabaki kwa muda gani itategemea ushauri wa madaktari wake."
Your browser doesn’t support HTML5
Hali ya afya ya Rais Kikwete inaendelea vizuri - Mbena
Kiongozi huyo kwa wakati huu anapumzika katika chumba chake cha hospitali iliyoko karibu km 50 kutoka mji mkuu wa Washington, na maafisa wa hospitali wanaeleza kwamba alianza kutembea kidogo leo asubuhi na jioni. .