Viongozi wanaohasimiana Msumbiji watia saini makubaliano ya amani

Rais Arnando Guebuza, kushoto, na kiongozi wa zamani wa waasi Afonso Dhlakama, kulia, wapeana mkono baada ya kutia saini makubaliano ya amani Maputo, Sept. 5, 2014.

Rais Amando Guedbuza wa Msumbiji na kiongozi wa kundi la zamani la waasi la Renamo, Afonso Dlakama wametia saini makataba wa kihistoria wa amani mjini Maputo siku ya Ijuma, na hivyo kufikisha kikomo miaka miwili ya ugomvi ulokumbusha enzi za vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Dhlakama aliwasili Maputo Alhamisi usiku baada ya kuwa mafichoni msituni kwa miaka miwili, na kutia saini makubaliano ya amani mbele ya wanadiplomasia na wageni wa heshima 100.

Your browser doesn’t support HTML5

Dhlakama awasili Maputo

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Idhaa ya Kireno anaripoti kwamba wageni walishangiria na kupiga makofi pale viongozi hao wawili walokua wakihasimiana kukubatana baada ya kutia saini mkataba wa kusitisha uhasama.

Kwa miaka miwili wanajeshi wa serikali wamekua wakipambana na wapiganaji watiifu na Dhlakama, huku kiongozi huyo wa waasi akiituhumu serikali kwa kukiuka makubaliano ya amani ya 1992, yaliyomaliza vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.