Kiongozi wa mashirika ya kiraia Kivu kaskazini aomba mkataba wa Addis Ababa uheshimiwe.

Maseneta sita wa Marekani watembelea Goma

Kiongozi wa mashirika ya haki za kiraia huko Kivu Kaskazini Bw.Mustafa Muiti amesema ameshangazwa na ziara ya ujumbe wa maseneta wa Marekani waliokwenda nchini humo kutokuweza kuonana nao na badala yake kukutana na viongozi wa serikali na Monusco pekee.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kiongozi huyo ameongeza kwamba ujumbe huo uliokwenda huko mwishoni mwa juma ulikutana na viongozi wa serikali na Monusco na kufanya nao mazungumzo ambayo walitoa ushauri wa kutafuta suluhu ya kidiplomasia .

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Mustafa Muiti




Amesema wazo hilo si baya lakini Congo ilikuwa ya kwanza kufanya mazungumzo, lakini mazungumzo baina ya viongozi wa DRC na M23 ni kuendelea kushikamana na kubuni njia za kuweza kufikia suluhu ya kudumu ili kuleta amani katika eneo ambalo limekumbwa na mapigano.

Kuhusu Marekani amesema angependa wawaambie Uganda na Rwanda waheshimu mkataba wa Adiss Ababa na pili kuwaambia Rwanda watoke katika ardhi ya Congo wanakowasaidia waasi wa M23 na pia angependa Rwanda wakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kundi la Fdlr ili waonyeshe wanakubaliana na diplomasia jambo ambalo litasaidia wale waliokimbia waweze kurudi nyumbani na wao waone amani na usalama kwa maendeleo ya kudumu.