Somalia ingali yahitaji msaada kutoka Jumuia ya Kimataifa: Mahiga

Rais anaeondoka madarakani Somalia Sharif Sheikh Ahmed akipongezwa na mjumbe maalum wa UM Augustine Mahiga

Rais mpya wa Somalia, Hassan Shiekh Mohamud anasiku thelathini ya kuteuwa serikali mpya inayotazamiwa kuwahusisha wajumbe kutoka Koo na sehemu mbali mbali za jamii.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Mjumbe maalum wa Umoja wa Matiafa kwa ajili ya Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema huu ni wakati muhimu kwani ni mara ya kwanza kwa Somalia kujipatia serikali isiyo ya mpito baada ya zaidi ya miaka 20.

Mahiga amesema "kiongozi mpya Bw. Mohamud ni mtu mwenye ujuzi na Wasomali wamempenda na wanamatarajio makubwa na ataleta mabadiliko na tofuati kubwa na hasa mageuzi katika mueleko katika nchi ya Somalia."

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na Balozi Mahiga


Akikubali kushindwa, rais anayeondoka, Ahmed Shariff, alisema kuwa huo ndio ulikuwa uchaguzi wa kwanza huru nchini Somalia kwa miaka 42 tangu Mohamed Siad Barre kuchukua mamlaka mwaka 1969.