Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa, alifanya ziara ya ghafla Ijuma Novemba 27, 2015 katika bandari ya Dar Es Salaam na kutangaza hatua za kuwafukuza maafisa waandamizi wa Mamlaka ya Mapato TRA, kutokana na ubadhirifu.
akifungua kikao cha kwanza cha bunge la 11 la Tanzania Rais Magufuli ameahidi kutekeleza ahadi alizotowa ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa hadi kulinda haki za raia.
Wagombea wataka mwenyekiti wa tume kukamilsha taratibu za majumuisho.
John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa rais Tanzania kwa kupata asilimia 58 kwa 40 za mpinzani wake Edward Lowassa. Upinzani umepinga matokeo hayo.
Mara tu baada ya upigaji kura kumalizika matatizo kadha yalizuka katika shughuli ya kuhesabu kura katika visiwa vya Zanzibar. ZEC haijatoa maelezo zaidi kuhusu kinachofuata baada ya uchaguzi kufutwa
Baadhi ya wagombea wa upinzani ambao wameingia katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge wameweza kuwaangusha mawaziri na manaibu mawaziri waliokuwa wakitetea majimbo yao ya uchaguzi.
Matokeo ya uchaguzi yameendelewa kutolewa siku nzima ya Jumatatu huku ikidhihirika kuwa wabunge kadhaa za zamani wameangushwa. Matokeo rasmi ya urais yangali yanaruhusiwa kwa hamu na wananchi.
Pandisha zaidi