Waziri wa Mambo ya Nje Israel Katz atahutubia Umoja wa Mataifa mchana kwa niaba yake.
Chirac alitumikia miaka miwili katika wadhifa wa urais wa Ufaransa na kuliongoza taifa lake kuingia katika sarafu moja ya Ulaya.
Rivlin anajukumu la kumchagua mgombea anayeamini kwamba ana fursa kubwa ya kuunda serikali ya umoja baada ya wote Netanyahu wala Gantz kutopata uungaji mkono unaohitajika kwa kupata wingi wa viti katika bunge la Israel
Utawala wa Trump ulisema kwamba mkataba kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani hayakufanya vya kutosha kuizuia Tehran kuendelea na utengenezaji wa silaha za nyuklia
Rais Paul kagame wa Rwanda alitoa matamshi hayo kwenye hotuba yake ya Jumanne kwa wajumbe wa kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York . Mkutano ambao hufanyika kila mwaka na kujadili masuala mbali mbali ikiwemo usalama, afya, elimu, mabadiliko ya hali ya hewa na mengineyo
Kwa miezi kadhaa spika Pelosi amesita kufungua mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Trump kufuatia shutuma za awali za kuingilia kati sheria kuchukua mkondo wake kutoka kwenye ripoti ya Robert Mueller juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani 2016.
Vyama vya upinzani mara moja vimemtaka waziri mkuu ajiuzulu na kikao cha bunge kuitishwa Jumatano.
Hotuba ya Trump, ambayo pia ililenga masuala mengine mbalimbali, pia iligusia uhamiaji, huku akisema sera zinazoungwa mkono na wanaharakati wa mipaka iliyo wazi, zinawaumiza raia na kuwa ni za kishetani.
Greta Thunberg : Sayansi imekuwa ikiweka wazi (athari za uharibifu wa mazingira) kwa miaka 30, lakini bado viongozi hawajachukuwa hatua za kutosha.
Wademocratic hao walisema wizara ya mambo ya nje Marekani imekiri kuwa ofisa mwandamizi wa Mike Pompeo alisaidia moja kwa moja kupanga mikutano kati ya mwanasheria wa Rais wa Marekani Donald Trump, Rudy Giuliani na maafisa wa Ukraine
Kitengo kinachopambana na ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC kinasema visa vingine 9 vya ugonjwa huo vimepatikana katika kijiji cha Butama.
Miezi kadhaa iliyopita, kampuni hiyo ilikuwa imeripoti kiwango kidogo cha watalii kutokana na mgogoro wa Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit)
Pandisha zaidi