Papa pia alitoa Baraka kwa waathirika wa ugonjwa wa Ebola kwa baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi hususani nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea pamoja na watu wanaotoa huduma za tiba.
Msemaji wa White House Josh Ernest, amewaambia wanahabari Alhamisi kwamba “siwezi kataa ziara ya Rais Castro.”
Katika mahojiano na ABC News, Rais Obama, amesema kwamba amemueleza Rais wa Cuba, Raul Castro, kwa njia ya simu kwamba Marekani itaendelea kuhamasisha demokrasia na kutetea haki za binadamu.
Uwamuzi wa Obama unafuatia mazungumzo ya siri ya karibu miezi minane yakiongozwa na Vatican, katika juhudi za kurudisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili na kubadilishana wafungwa wa ujasusi kati ya nchi hizi mbili.
Kundi la wafanyakazi wa bunge, wengi wao wakiwa Wamarekani weusi takriban 150 walikusanyika kwenye ngazi za jengo la bunge muda mfupi baada ya saa tisa na nusu alasiri konyesha mshikamano wao na waandamanaji , katika kile kiongozi wa dini bungeni Barry Black alichosema ni ‘Sauti ya wale wasiosikika’.
Pia anatarajiwa kuzungumza kwenye mkutano wa Benki ya Dunia juu ya biashara haramu ya pembe za ndovu, faru na sehemu nyingine za mnyama ni “moja ya chanzo kikuu cha rushwa na uhalifu duniani hii leo
UNAIDS hivi sasa ina kile inachokiita mkakati wa FAST TRACK wa kumaliza mlipuko huu ifikapo mwaka 2030. Awamu ya kwanza inaweka malengo kwa mwaka 2020 ambayo inajulikana kama 90-90-90
Ghasi hizo zinafuatia tangazo la mwendesha mashitaka wa kitongoji cha Missouri Robert McCulloch kwamba jopo hilo halikuona sababu yoyote ya kumfungulia mashitaka polisi huyo Darren Wilson.
Ni mrepublican pekee katika baraza la mawaziri la bwana Obama. Gazeti la The New York Times linawakariri maafisa waandamizi katika utawala wakiripoti kujiuzulu huko kunatokana na shinikizo kufuatia kuongezeka kwa migogoro kadhaa kwenye sera za mambo ya nje
Katika hotuba kwa taifa, rais alifafanua mpango wake wa kuidhinisha amri ya rais juu ya mageuzi ya uhamiaji itakayozuia kwa muda kurudishwa nyumbani wahamiaji milioni 5 wanaoishi nchini kinyume cha sheria.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, alimtaja mfaransa huyo kuwa ni Maxime Hauchard, mwenye umri wa miaka 23, aliyekwenda Syria, zaidi ya mwaka mmoja uliopita, kama mfanyakazi wa huduma za dharura
Pandisha zaidi