Wakati basi hilo lilipopita mji wa Rhotia Hill, likiwa katika kasi likishuka mlima kuja katika makutano ya barabara ya Kwa-Karani,' walioshuhudia ajali hiyo waliona basi likipaa angani na kutumbukia katika korongo refu pembeni ya Mto Marera wilayani Karatu.
Lakini maafisa wa Marekani wanasisitiza kuwa Trump hapingi kuwepo kwa mataifa mawili; wanasema kuwa kwa ufupi anaweka njia zote mbadala wazi na kuwaruhusu Waisraeli na Wapalestina kujiamulia wenyewe ni vipi wanataka mazungumzo ya amani yachukue mkondo wake.
“Tuliwasaidia kuwaleta wanajeshi wa Somalia kwa kutumia ndege zetu, na sisi tulikuwa tuko mbali nyuma kabisa wakati wakiendelea na operesheni hiyo dhidi ya al-Shabab,” Davis amesema akiwa Wizara ya Ulinzi Marekani. “Hapo ndipo majeshi yetu yaliposhambuliwa.”
Baadhi ya vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa hii ni ishara tosha ya hatari iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa kuhudumiwa na watalaam feki na jinsi isivyokuwa sahihi kwa watu hawa kutetewa.
Anaeshikilia rekodi ya dunia kwa sasa ni Dennis Kimetto kutoka Kenya alishinda kwenye mbio za Berlin Marathon 2014.
Ikulu ya White House hivi sasa inakabiliwa na kazi ngumu ya kuweza kushawishi muswada wa Afya kupitishwa kwa kura ambazo ni za chache zaidi katika Seneti.
Mchumi wa kilimo Paul Makube, ambaye anafanya kazi na First National Bank ya Afrika Kusini, ameiambia VOA inaleta tija kuzungumzia kuhusu kilimo wakati panapo zungumziwa kujenga masoko yenye ushindani, na kuboresha ubunifu na teknolojia.
Aidha Waziri wa Habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo tayari wamekamatwa.
Wakati akimaliza kuongea na kupeana mkono na Trump, Abbas aliongeza kusema kwa Kiingereza: “Sasa, Rais, kwa kushirikiana na wewe, tunamatumaini.”
Moja ya masuala yaliyojadiliwa ni jinsi vyombo vya habari vitaendeleza uhuru wake na jinsi taasisi za mawasiliano zinavyotakiwa kubuni mkakati thabiti wa kutema habari ghushi au bandia zinazozidisha migogoro katika jamii.
Trump amesema anataka kuleta wafanyakazi “bora na mahiri zaidi” wa kigeni na kuzifanyia marekebisho sheria za uhamiaji zinazohusiana na kazi na usalama wa mpakani.
Jeshi la anga la Marekani limesema katika taarifa yake ndege hizo za mashambulizi zilikuwa zimeruka kutoka Guam kwa ajili ya kufanya mazoezi na majeshi ya anga ya Korea Kusini na Japan.
Pandisha zaidi