Wakati uwezo wa uchumi wa China umepanuka na ushawishi wake umekua duniani, Beijing inatafuta njia kusahihisha kile inachokichukulia kuwa ni upotoshwaji wa sura yake halisi.
Mkutano wa Jumatatu katika Oval Office unaangaliwa kwa makini mjini Cairo ambapo kunashauku kubwa juu ya kusudio la Trump kwa nchi ya Misri na ulimwengu mkubwa wa Kiislamu kufuatia katazo la Trump kwa raia wa nchi sita zenye Waislamu wengi kuingia Marekani.
“Sasa tunashangaa rais ameruhusu wafanyabiashara kama sisi wako barabarani, lakini sisi wafanyabiashara wadogo tuliovumilia miaka yote, miaka sita tuko hapa, hili jengo linaitwa machinga complex sasa tumekuja wamachinga wenyewe tunatolewa.
Seylici amesema “Sisi tunaikaribia njaa, tathmini tuliofanya na ile iliofanywa na mashirika ya misaada inaonyesha njaa iko karibu kutangazwa upande wa mashariki ya eneo la Somaliland,
Katibu mkuu wa TABOA Eneo Mrutu amesema sheria inayolengwa kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva kusababisha mmiliki kufungwa jela.
Ofisi ya Vyombo vya habari ya Dubai imesema moto huo ulizuka katika eneo la Address Residences Fountain Views towers, na kuwa wazima moto wameweza kuudhibiti.
“Iwapo mtu angeniambia huko nyuma kwamba nilikuwa naweza kuwa na nafasi ndogo ya kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel, ningelifikiria kuwa ni fursa iliyo nadra sana kama vile kujikuta nimesimama katika mwezi,” amesema Bob Dylan.
Marehemu amekuwa mstari wa mbele kuwatumikia watanzania tangu akiwa mwanachama wa kawaida, kabla hajawa Mjumbe wa Kamati Kuu na kisha Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema Mbowe.
Kwa kauli moja wanachama wote 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamekubaliana kwamba Monusco pamoja na intervention brigade force lazima vipewe uwezo zaidi ili kupambana na hali hii mpya.
Laetitia Bader, mtafiti wa shirika la haki za binadamu (Human Rights Watch) anaehusika na Somalia, ametadharisha kuwa lazima mashambulizi hayo yafanyike kwa uangalifu sana, hasa ikizingatiwa hali ya ukame inayoendelea nchini humo.
“Wizara inapenda kuwafahamisha kuwa habari za mitandaoni ni za uongo na zinakusudia kuchafua sifa ya Rais Magufuli ambayo amejitengenezea kwa kipindi chote na sura nzuri ya Tanzania kwa ujumla,” taarifa ya wizara imeeleza.
Kamanda wa Polisi eneo la Pwani Philip Tuimur amewaambia waandishi wa habari kuwa, waliokamatwa ni pamoja na raia 3 wa Italy, raia mmoja wa Mauritius, Mtanzania mmoja na Wakenya 8 wakiwapo wanawake wawili.
Pandisha zaidi