Viongozi wa upinzani nchini Kenya, chini ya Muungano wa kitaifa wa National Super Alliance (NASA), wanatarajiwa kutangaza yule atakayepeperusha bendera yao wakati wowote sasa, kufuatia mikutano mingi ambayo imekuwa ikifanyika kwenye miji mbali mbali
Stephens alikuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa sana na polisi na kulitolewa zawadi ya dola 50,000 kwa mtu atayeweza kutoa taarifa zake zitazowezesha kukamatwa kwake.
Serikali inalichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa na kwa utofauti mkubwa kuweza kuhakikisha inarejesha hali ya kawaida katika maeneo ambayo uhalifu umekuwa ukijitokeza na kujirudiarudia, amesisitiza Waziri Nchemba.
Mbunge Bitekko ameeleza kuwa wananchi wa Tanzania kwa sasa kwa matukio ya mauaji ya polisi wanahofu na usalama wao, maisha yao na mali zao kutokana na matendo haya ya kinyama.
Hata hivyo wakati anaelekea katika milima ya Newton, Edna Kiplagat akaongeza kasi kufikia ushindi katika muda (usio rasmi) wa masaa 2, dakika 21, sekunde 53 katika mbio hizo za 121, siku ya Jumatatu.
Lakini kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi hilo Brigedia Richard Karemire hiyo ni hatua ya kawaida nakusema “Tutakuwa na uwezo wa kuwastaafisha zaidi ya maafisa 2000, wakiwemo majenerali,”
Uongozi wa Trump umejikita katika kuweka vikwazo madhubuti vya kiuchumi, kuhusisha kuzuia mafuta kuingia nchi hiyo, kupiga marufuku shirika la ndege la nchi hiyo kimataifa, kukamata meli za mizigo na kuziadhibu Benki za China.
Makamu wa Rais Mike Pence, ambaye alikuwa njiani kuelekea Korea Kusini jioni Jumamosi alipewa muhtasari wa kufeli kwa jaribio hilo la kombora na amezungumza na Rais Donald Trump kama ilivyoeleza taarifa ya ofisi yake.
Sakata la kughushi vyeti limekuwa kubwa baada ya mmoja wa wateule wa Rais Magufuli, ambaye hivi sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kushutumiwa kuwa anatumia 'vyeti vya kughushi' baada ya kufeli elimu ya sekondari..,
Profesa Kabudi baada ya kufika mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, akiwa katika nafasi ya uwaziri alisema hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, akiwemo Waziri Mkuu.
Jeshi la Polisi limetoa maelezo juu ya sababu ya kuwepo mauaji ya askari katika maeneo ya Mkuranga, Rufiji, Ikwiriri na Kibiti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, amesema hakubaliani na Zitto kuwa ni sawa kwa Bunge kumkubalia yeye kuwasilisha hoja yake binafsi ili ijadiliwe.
Pandisha zaidi