Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema iko haja ya kulidhoofisha kundi la al-Shabab linaloendelea kufanya mashambulizi kwa muongo mmoja, na kuliwezesha Jeshi la Umoja wa Afrika kulitokomeza kundi hilo.
Kiongozi mkongwe wa dunia anasema chama kimemtaka agombaniye kiti cha rais katika uchaguzi ujao, lakini kikihisi inabidi astahafu yeye yuko tayari na hivyo chama kinabidi kuitisha mkutano mkuu kumchagua kiongozi mpya.
Ziara ya mawaziri wa Marekani Mexico ilikusudia kuainisha matakwa ya amri ya kiutendaji ya Rais Trump ya January 25 juu ya uhamiaji ambapo maelezo yalikuwa ni kuwaondoa kwa haraka wahamiaji wote walio haramu nchini Marekani.
“Chama cha waandishi kimepinga vikali namna ambavyo utoaji habari usio rasmi "gaggle" unavyo endeshwa na White House,” amesema Jeff Mason, Kiongozi wa Umoja huo ambaye anafanya kazi na shirika la habari la Reuters.
Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) limesema kuna wasiwasi mkubwa wa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kuelekezwa dhidi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini.
“Katika kipindi hiki cha huzuni na masikitiko, fikra zangu na dua zangu nazielekeza kwa familia ya marehemu, ndugu na marafiki. Ni maombi yangu Mwenyezi Mungu Mtukufu awapeni nguvu katika kusubiri,” Kenyatta amesema.
Profesa Nabhany alizaliwa tarehe 27 Novemba 1927 huko Lamu na baadaye kuhamia mjini Mombasa kwa shughuli za kikazi.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema mwaka 2016/17 uligubikwa na wimbi la uvunjifu wa haki za binadamu.
Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Luis Videgaray amesema nchi yake haitokubali pendekezo jipya kuhusu wahamiaji lililotengenezwa na Marekani “peke yake” na hawatosita kupeleka suala hilo Umoja wa Mataifa.
“Wananchi wa Somalia wametoa kauli yao na wana matumaini makubwa juu ya serikali yao mpya katika kulijenga na kuliendeleza taifa hilo,” Rais Uhuru Kenyatta amesema.
“Matatizo ambayo Somalia inapitia imekuwa ni malimbikizo ya migogoro ya zaidi ya miaka 20, na ili kutatua matatizo yote haya inaweza kuchukua zaidi ya miaka 20 mingine,” Rais Farmajo amesema.
Msemaji wa White House aligusia baadhi ya malalamiko ya Trump kuhusu vyombo vya habari akijibu swali la mwandishi, alotaka kujua iwapo rais “ana majuto yoyote juu ya kauli yake au ufafanuzi katika shutuma” dhidi ya vyombo vya habari kwa kuwaita “maadui,”
Pandisha zaidi