Baadhi ya idara mbalimbali za serikali ya Marekani zilizo kuwa zimefungwa kwa siku 35 zimefunguliwa Jumamosi, siku mbili kabla ya Idara ya Mapato ya Ndani (IRS) kuanza kushughulikia mchakato wa kupokea mawasilisho ya kodi za wananchi kwa mwaka 2018.
Kongamano la Uchumi Duniani (World Economic Forum) lililokuwa linafanyika Davos, Switzerland, limemalizika Ijumaa, na ilikuwa wazi kwamba viongozi muhimu akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump hawakuhudhuria.
Katika tamko lake, kampuni ya NSO ya Israeli ilikanusha kuwa kwa namna yoyote ile inahusika na operesheni ya ujasusi huo unaolenga wanazuoni na watafiti wa Citizen Lab,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amemchagua mzoefu wa sera za kigeni Elliott Abrams kuwa mjumbe maalum atayeshughulikia masuala ya sera ya Marekani juu ya Venezuela,
Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kufunguliwa kwa idara za serikali kuu ambazo zilifungwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya kufikia makubaliano na kamati ya pamoja ya bunge.
Katika utetezi wake, Tido alidai kuwa mchakato mzima wa kuingia ubia wa kuhamisha TBC kutoka katika mfumo wa analojia kwenda digitali ulifanywa na bodi ya TBC.
Rais wa Marekani Donald Trump amemuonya Maduro Alhamisi kuwa “hatua zote zinazoweza kuchukuliwa ziko mezani”...
Stone ataletwa katika mahakama ya serikali kuu huko Fort Lauderdale, Florida, baadae siku ya Ijumaa, ofisi ya Mueller imeeleza.
Rais Maduro ametangaza anasitisha mahusiano ya kidiplomasia na Marekani, akijibu tangazo la Rais Donald Trump kwamba anamtambua rasmi Guaido kuwa ni Rais wa muda wa Venezuela.
Tshisekedi alondolewa jukwaani akiwa hajisikii vizuri alipokuwa akitoa hotuba yake baada ya kuapishwa na hivyo kuketi chini.
Korea Kaskazini inajiandaa kwa mkutano wa pili kati ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un na Rais wa Marekani Donald Trump.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Alhamisi imemuapisha kiongozi wa upinzani kuwa ni rais mpya ambaye hakutarajiwa kuchaguliwa, ikiwa ni hatua ya kukabidhiana madaraka kwa mara ya kwanza kwa njia ya amani na demokrasia katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati tangu ijipatie uhuru miaka 60 iliyopita.
Pandisha zaidi