Mattis alituma ujumbe wa heri kwa majeshi yote ya Marekani dunia nzima, akipongeza kazi wanazofanya kwa kusema “wao ndio macho na walinzi wa taifa hili” akiahidi kufanya juhudi zake zote “kuhakikisha majeshi yetu yako tayari kupambana leo na siku za usoni.”
Wanawake wanathibitisha kuwa kuweza kupata ushauri wa uzazi wa majira na kupata matibabu kinamama kumechangia zaidi ya kitu chochote kile katika kumwezesha mwanamke katika karne hii ya 20 na tunakokwenda katika karne ya 21 pia.
Rais Donald Trump amesema kuwa ataanzisha “dira mpya” kwa taifa la Marekani ambayo itawajali wafanyakazi ambao wametelekezwa kwa sababu ya kufungwa kwa viwanda na uchumi kutetereka.
Ubalozi wa Marekani nchini Gambia umefungwa kwa sababu kuna uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani katika nchi hiyo.
Sean Spicer, ambaye atakuwa Msemaji wa Trump katika ikulu ya White House, amesema rais mteule amekuwa akiendelea kufanya mabadiliko katika hotuba yake ya kuapishwa ambayo ataitoa katika ngazi za Bunge la Marekani mchana wa siku ya Ijumaa.
Album yake mpya ya kuwaaga wapenzi wa muziki wake inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.
Donald Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani kuanzia Januari 20, atakapoapishwa rasmi katika ngazi za Bunge la Marekani kuongoza nchi hii wakati mamilioni ya watu wakimwangalia kupitia luniga ulimwengu mzima.
Katika ujumbe wake wa taifa moja bila ya ubaguzi, Obama amesema kwamba anategemea siku za usoni kuona mwanamke, mlatino, myahudi, Mhindu wote wanakuwa marais na wengi wengineo hapa Marekani.
Bwana Chebukati pamoja na makamishna sita wameidhinishwa na bunge la kitaifa kuiongoza tume hiyo wakati Kenya inajiandaa kwenda kwenye uchaguzi mkuu miezi michache ijayo.
Rais George WH Bush amepata nafuu baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wanaridhishwa na hali yake jinsi inavyoendelea hivi sasa.
Kulikuwa hakuna ripoti za majeruhi lakini mtikisiko ulifika hadi Rome, ambako vituo vya treni vilifungwa kama tahadhari na wazazi walitakiwa kuwafuata watoto mashuleni.
Washington ni jiji lililo katika mpito wiki hii, wakati Rais Barack Obama akijiandaa kukabidhi madaraka kwa mrithi wake, Rais mteule Donald Trump.
Pandisha zaidi