Mzee Ngombale-Mwiru alikuwa kiongozi wa sera na kanuni katika chama cha mapinduzi kwa muda mrefu. Aliaminika sana na mwasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere ambaye alimteua kushika nafasi kadha katika baraza la mawaziri na ndani ya CCM
Meli ya MV Hoeg Transporter ilikamatwa katika bandari ya Mombasa Septemba 17 baada ya kukutwa na shehena kubwa ya silaha. Silaha hizo imethibitishwa zinaelekea DRC kwa majeshi ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa.
Waalimu walikuwa katika mgomo kwa zaidi ya mwezi mmoja wakidai serikali iongeze mishahara kwa kiasi cha asilimia 50 kama iliyoamriwa na mahakama hapo awali. Serikali imesema haina uwezo wa kuongeza mishahara kwa kiwango hicho.
Rais Jakaya Kikwete atahutubia bunge la Kenya wiki chache kabla hajaondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania. Anatazamiwa kusisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kujenga shirikisho la nchi za Afrika Mashariki.
Baada ya viongozi wa upinzani kushindwa kuamua nani kati yao awe mgombea wa umoja kupambana na rais Museveni kila mmoja ameamue kwenda kivyake. Wanasiasa wengine wengi wanaingia kama wagombea binafsi.
Zikiwa zimebakiwa chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania tume ya uchaguzi inasema iko tayari kwa uchaguzi huru na wa haki nchini humo.
Zaidi ya mahujaji 1,000 walifariki katika mkanyagano Mina wiki iliyopita. Mahujaji wengi wameanza kurejea katika nchi zao na madai na maelezo zaidi yameanza kujitokeza kutokana na mkasa huo.
Brigedia Jenerali, Gilbert Diendere alizungumza siku moja baada ya wanajeshi kuiangusha serikali ya muda akisema jeshi lilipanga mapinduzi kwa sababu utaratibu wa kisiasa nchini humo haukuwa haki
De Greiff anasema amewasilisha wasiwasi wake kwa baraza la haki za binadam la umoja mataifa kwa matarajio nchi kuwa nchi wanachama watafahamu ukubwa wa hali inayojitokeza nchini Burundi na kuchukuwa hatua ili kuepuka janga kutokea.
Wafuasi wa Mbabazi, walikaidi hatua ya polisi kuwarushia mabomu ya machozi ili kuwatawanya. Waziri mkuu huyo wa zamani amekuwa akivutia makundi makubwa ya watu katika mikutano yake ya awali.
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye.
Pandisha zaidi