Uchaguzi Kenya 2017
Ripoti Maalum: Uchaguzi Kenya 2017
Maoni
Unadhani Uchaguzi Wa Kenya Utakuwa Wa Amani
This poll has been already closed
Maoni
Ni suala gani litaamua kura yako katika uchaguzi Kenya?
This poll has been already closed
Kuhusu Mradi Huu
Kuhusu Mradi Huu Waandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA wameandaa Makala Maalum juu ya Uchaguzi Mkuu Kenya baada ya kuzungumza na wananchi katika ngazi mbalimbali wakati kampeni zinaendelea nchini humo. Ukurasa huu unaangazia mchakato mzima wa uchaguzi ambao utafanyika Agosti 8, 2017. Wagombea urais wanane kutoka vyama mbalimbali nchini Kenya wameelezewa kwa ufupi katika muhtasari wa ripoti hii maalum ya uchaguzi. Pia tutakuletea makala mbalimbali zikiangaza ilani za uchaguzi namna zinavyoahidi kupambana na ufisadi, kuleta maendeleo ya uchumi, usalama, elimu, afya. Pia tunaangalia vinyang’anyiro vya ugavana kama moja ya sehemu muhimu ya uchaguzi huu, pamoja na kuangalia vipaumbele vya vyama katika makundi maalum kama vile wanawake, vijana na mikakati ya kukabiliana na ukabila.
Walio Tayarisha Makala Hizi
Utangulizi na muhtasari: Jaffar Mjasiri
Maswala:
Ufisadi – Jaffar Mjasiri
Uchumi – Kennedy Wandera
Usalama – Josephat Kioko
Elimu – Sunday Shomari
Afya – Mary Mgawe
Wanawake – Salma Muhamed
Vijana - Colyns Liberty
Ukabila – BMJ Muriithi
Wasifu:
Raila Odinga – Mwamoyo Hamza
Uhuru Kenyatta – Idd Ligongo
Wagombea Urais Wengine - BMJ Muriithi
Magavana: Josephat Kioko
Vyama vya Siasa: Harrison Kamau