Mkutano Mkuu wa UN unafanyika wakati dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali

Your browser doesn’t support HTML5

Suala la kwanza kwenye orodha hiyo, ni Gaza. Hapa, msimamo wa Marekani hauwiani na wa wajumbe wengine kwenye baraza hilo, ambalo wiki iliyopita lilipitisha kwa wingi wa kura, azimio la kuitaka Israel ikomeshe hatua ya kukalia kwa mabavu eneo la Palestina ndani ya miezi 12 ijayo.

Marekani ilikuwa miongoni mwa nchi 14 zilizopiga kura ya "hapana", ambazo Thomas-Greenfield alisema ziliendana na msimamo wa Washington kuhusu "hatua za upande mmoja ambazo zinadhoofisha matarajio ya suluhisho la serikali mbili."