Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 04:13

Zoezi la utoaji chanjo za polio Pakistan lakubwa na ghasia


Mfanyakazi wa afya akitoa chanjo ya polio kwa mtoto mjini Lahore, Pakistan, Sept. 9, 2024.
Mfanyakazi wa afya akitoa chanjo ya polio kwa mtoto mjini Lahore, Pakistan, Sept. 9, 2024.

Makundi ya wanamgambo yameongeza mashambulizi dhidi ya timu zinazotoa chanjo za polio, pamoja na polisi wanaowalinda nchini Pakistan, licha ya kuzuka kwa kesi mpya za maambulizi ya ugonjwa huo nchini.

Maafisa wanasema kwamba kutokana na kudorora wa usalama, timu za utoaji chanjo zinashindwa kufikia jamii zilizopo kwenye hatari zaidi ya janga la polio. Jumanne, wanamgambo walishambulia vituo viwili vya afya kwenye wilaya za kikabila za Orakzai na Waziristan, ambazo zinatumika kwenye kampeni ya utoaji pilio nchini.

Afisa wawili wa polisi waliuwawa kwenye shambulizi hilo kwenye eneo hilo lililo ndani karibu na mpaka wa Afghanistan. Kulingana na maafisa kwenye wilaya ya Waziristan, wanamgambo walipokonya bunduki kutoka kwa maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda timu za utoaji chanjo, na kisha kuonya wafanyakazi wa afya dhidi ya kushiriki zoezi hilo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Mohsin Naqvi, akizungumza kupitia taarifa baada ya matukio hayo alisema,”Mashambulizi dhidi ya timu za polio, pia ni shambulizi kwenye usalama wa Pakistan.” Hali ya taharuki imetanda kote nchini Pakistan miongoni mwa wafanyakazi wa afya wanaotoa chanjo za polio.

Forum

XS
SM
MD
LG