Hilo limejiri huku wengine takriban 2,000 wakipata majeraha kutokana na vifaa vya aina nyinginezo, kulingana na ripoti iliyotolewa Jumatano. Utafiti uliofanywa na shirika la madaktari la Haki za Binadamu pamoja na lile la Mtandao wa kimataifa wa Uhuru wa Kijamii, kwa ushirikiano na lile la utafiti la Omega ulichukua miaka miwili na nusu kufikia ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ni kutokana na data za majeruhi kutoka kwa vituo vya afya, yaliosababishwa na polisi kote ulimwenguni kwenye mataifa kama vile Colombia, Chile, Hong Kong, Uturuki na kwenye maandamano ya Black Lives Matter hapa Marekani, miongoni mwa sehemu nyingine. Data nyingi zilikusanywa baada ya watu kukimbizwa hospitalini kufuatia kujeruhiwa kwenye maandamano, na kuorodheshwa na wahudumu wa afya.