Hiyo ni moja mkati ya matukio ya mwisho wa wiki katika mapigano yaliyoanza mwezi Aprili, baina ya jeshi la taifa linaloongozwa mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, na naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza kikosi cha akiba cha RSF.
Taarifa ya kamati ya wanasheria inayotaka demokrasia imesema mashambulizi yamefanyika katika soko la Omdurman, wakati wa mashambulizi ya kufyatuliana risasi baina ya pande hizo mbili.
Taarifa iliyotumwa na kamati hiyo inayo orodhesha matendo ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika mgogoro huo, kwenda kwa shirika la habari la AFP, imesema kwamba zaidi ya raia 20 wameuwawa na wengine kujeruhiwa.
Siku ya Jumamosi vyanzo vya afya vinasema shambulizi katika nyumba mjini Khartoum limeuwa raia 15.
Forum