Shambulizi hilo limetokea kwenye kijiji cha Albu Bali karibu na mji wa Khalis takriban kilomita 80 kaskazini mwa Baghdad, polisi wameongeza. Wanavijiji walitumia magari yao binafsi kuwapeleka majeruhi hospitali wakati maafisa wa afya wakisema kwamba miili ya watu waliokufa ilikuwa na majeraha ya risasi.
Wameongeza kusema kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwa kuwa baadhi ya majeruhi wapo katika hali mahututi. Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika, lakini polisi mjini Khalis wanashuku kundi la kigaidi la Islamic State lilihusika. Shambulizi hilo limetokea siku moja baada ya bomu la kando ya barabara kuua polisi 9 karibu na mji wa kaskazini wa Kirkuk, Jumapili.
Facebook Forum