Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:25

Watu wapotea mikononi mwa mamlaka za Kenya


Shirika la haki za binadamu “Human Right Watch” linaeleza darzeni ya watu wamepotea na hawajulikani walipo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wakiwa mikononi mwa vikosi vya kukabiliana na ugaidi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vikosi vya jeshi vimewakamata karibu watu 34 waliohusishwa na kundi la kigaidi la al-Shabab lakini hakuna yoyote kati ya hao aliyefunguliwa mashitaka.

Wanafamilia wanasema hawajui pale ndugu zao waliokamatwa walipo, licha ya ripoti kwamba walipotea wakiwa mikononi mwa maafisa.

Katika kipindi hicho pia, maiti 11 wa watu waliokuwa wamekamatwa awali na idara za serekali walipatikana, na kuongeza hofu kwa wale ambao hawajulikani walipo hasa ikizingatiwa hakuna maelezo kwa mujibu wa aangalizi wa haki za binadamu.

Juhudi za kupambana na ugaidi nchini Kenya ziliongezeka baada ya mashambulizi ya Aprili mwaka 2015 katika chuo kikuu cha Garissa yaliyosababisha vifo vya watu 147 wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

XS
SM
MD
LG