Taarifa za habari zinasema watu 120 wameuwawa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofuatana yaliyolenga ofisi za polisi na majengo ya serikali katika mji ulio kaskazini – Kano huko Nigeria.
Mji huo ulio na waislamu wengi uko chini ya amri ya kutotoka nje ya masaa 24 kufuatia shambulizi la ijumaa linalodaiwa kufanywa na kundi la waislamu wenye msimamo mkali la Boko Haram.
Msemaji wa Boko Haram amewaambia waandishi wa habari kwamba shambulizi la mabomu ni la kulipiza kisasi baada ya kukamatwa kwa wanachama kadhaa wa kundi hilo.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti pia kulikuwa na milipuko katika mji wa kusini wa Yenagoa kufuatia shambulizi la Kano lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Nigeria imegawanyika kati ya upande wa kusini wenye wakristo wengi na waislamu walioko kaskazini imeshuhudia ghasia za kiholela zilizoenea sana katika miezi ya hivi karibuni.