Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 20:58

Watu kadhaa wajeruhiwa katika mlipuko Burundi


Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi

Watu kadhaa wanaripotiwa kujeruhiwa katika milipuko ya mabomu yaliyotokea Jumanne jioni katika mji mkuu wa kibiashara wa Burundi Bujumbura.

Shuhuda aliyekuwapo katika eneo la tukio ambaye amezungumza na VOA kwa sharti la kutotajwa jina ameongeza kusema kuwa mabomu yalilipuliwa katika kituo kikuu cha mabasi katikati mwa jiji la Bujumbura.

Inaripotiwa tukio hilo lilitokea kati kati ya jiji la Bujumbura na maeneo ya kuzunguka yalizingirwa na Polisi kwa ajili ya kutuliza usalama na wananchi wanaripotiwa kuwa katika hali ya wasi wasi.

Sehemu iliyopata maafa makubwa ni kati kati ya soko la zamani la Bujumbura kwasababu ni sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi ambapo wanakusanyika kwa ajili ya kutafuta usafiri wa kwenda maeneo mbali mbali.

Shuhuda aliyekuwapo eneo hilo ameongeza kusema kuwa hali ni ya wasi wasi lakini Polisi hawakupatikana kuthibitisha taarifa juu ya tukio hilo.

XS
SM
MD
LG