Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 03:28

Watu 14 wauwawa kwa kupigwa na radi kwenye  kambi ya wakimbizi Uganda

Wakimbizi wapya wanaowasili wakitembea katika kituo cha mapokezi ambapo watasajiliwa kama wakimbizi katika Makazi ya Wakimbizi ya Rwamwanja katika Wilaya ya Kamwenge, Uganda Oktoba 21, 2024
Wakimbizi wapya wanaowasili wakitembea katika kituo cha mapokezi ambapo watasajiliwa kama wakimbizi katika Makazi ya Wakimbizi ya Rwamwanja katika Wilaya ya Kamwenge, Uganda Oktoba 21, 2024

Watu 14 waliuwawa kwa kupigwa na radi kwenye  kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda, polisi walisema leo Jumapili.

Watu 14 waliuwawa kwa kupigwa na radi kwenye kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda, polisi walisema leo Jumapili.

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi katika wilaya ya Lamwo. Msemaji wa polisi Kituuma Rusoke alisema watu wengine 34 walijeruhiwa. Waathirika bado hawajatambuliwa, aliongeza.

Wakazi katika kambi ya Palabek ambayo kimsingi inawahifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini, walikuwa wakihudhuria ibada katika jengo la muda la mabati wakati radi ilipopiga.

Radi mbaya kwa kawaida huripotiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki wakati wa misimu ya mvua. Rusoke alisema hakuna taarifa ya moto kuzuka kufuatia radi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG