Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi limesema mapigano mengine mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamelazimu zaidi ya raia laki moja kutoroka nyumba zao katika miezi miwili iliyopita.
UNHCR imesema ijumaa inawasiwasi sana kuhusu matokeo ya mapigano yaliyojumuisha majeshi ya serikali , majeshi ya waasi na wanamgambo wanaopingana yamekuwa magumu kwa raia.
Msemaji wa shirika hilo Adrian Edwards amesema eneo hilo linajumuisha majimbo ya kivu kaskazini na kusini .
Amesema takriban watu 22 wameuwawa na idadi ya wanawake kadhaa kubakwa.
Juhudi za umoja wa mataifa na serikalia ya Congo kuwaandikisha waasi katika jeshi na kuweka uthabiti katika eneo zimeshindwa.
Waasi wa kihutu kutoka Rwanda, au – FDLR, wameshutumiwa kwa kufanya uhalifu katika eneo hilo.
Waliwasili mashariki mwa Congo baada ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 ambako wahutu wenye siasa kali waliwauwa takriban watu 800,000.
Watu 100,000 watoroka mapigano mashariki mwa Congo

UNHCR imesema ijumaa inawasiwasi sana kuhusu matokeo ya mapigano yaliyojumuisha majeshi ya serikali , majeshi ya waasi na wanamgambo