Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:25

Watu 10 wakamatwa kuhusika na shambulio la Arusha


Shambulio la bomu Arusha, Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:03 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
Serikali ya Tanzania imetoa taarifa ya awali juu ya shambulizi la bomu katika kanisa katoliki la Mt.Joseph parokia ya Olacity mjini Arusha.

Akitoa kauli hiyo ya serikali bungeni Dodoma Jumatatu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Dr.Emmanuel Nchimbi aliwasihi wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiwasaka wale waliofanya shambulio hilo.

Maafisa nchini Tanzania wamewakamata watu 10 ikiwa ni pamoja na raia wanne wa Saudia Arabia .

Shambulizi hilo lilitokea wakati kanisa hilo jipya lilipofanya misa yake ya uzinduzi iliyohudhuriwa na balozi wa Vatikan nchini Tanzania .

Mashahidi kutoka kwenye eneo la tukio wanasema guruneti lilirushwa kwenye umati wa watu karibu na mlango wa kuingilia kanisani.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametangaza kukamatwa kwa watu hao siku ya jumatatu.

Hali katika hospitali ya Mount Meru Arusha ilikuwa tete huku madaktari wakifanya kila wawezalo kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kwa wakati mmoja. Sauti ya Amerika ilizungumza na Daktari Haika Mhando wa Mount Meru na kutaka kujua hali hospitalini hapo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG