Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:32

Watano wauwawa katika shambulizi Somalia.


Raia wa Somalia wakiangalia gari lililolipuliwa kwa bomu katika mji mkuu Mogadishu.
Raia wa Somalia wakiangalia gari lililolipuliwa kwa bomu katika mji mkuu Mogadishu.

Mizinga iliyokuwa imeelekezwa Ikulu yaenda kuangukia kwenye kambi ya waliopoteza makazi yao.

Watu wapatao watano waliuwawa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu wakati waasi waliporusha mizinga kuelekea jumba la rais lakini badala yake ikapiga kambi ya watu waliokimbia makazi yao.

Watu wengine 7 walijeruhiwa katika shambulizi hilo la usiku ambalo kundi la wanamgambo la Alshabab lilidai kuhusika.

Kanali mmoja wa jeshi la Somalia aliiambia Sauti ya Amerika kwamba shambulizi hilo halikuathiri Ikulu ya rais.

Hii ni mara ya pili katika wiki moja alshabab wamejaribu kushambulia ikulu ya rais.

XS
SM
MD
LG