Afisa wa jeshi nchini Ivory Coast amesema watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wameua watu watano na kujeruhi wengine kadhaa katika shambulizi la usiku katika mji mmoja katika eneo lisilo na utulivu kusini magharibi karibu na mpaka na Liberia.
Afisa huyo asiyetajwa alisema jumatano shambulizi hilo la saa mbili lilitokea katika mji wa ndani wa Sakre na kwamba maafisa wa jeshi walikamata watu kadhaa waliohusika katika shambulizi.
Mashahidi wanasema washambuliaji waliwasha moto nyumba kadhaa na maduka kuporwa. Madai yao hayakuweza kuthibitishwa na chombo huru.