Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:57

Wanamazingira wazungumzia uchafuzi wa plastiki, wataka mkataba kupitishwa

Mwanaharakati akiwa pamoja na waandamanaji wanaotaka "plastiki izuiliwe kutumika" katika viwanja vya BEXCO, ukumbi ambao Kamati ya UN ya Mazungumzo ya Kiserikali kuhusu Uchafuzi wa Plastiki (INC-5) yaliyofanyika huko Busan Novemba 25, 2024.

Wanaharakati kutoka makundi mbalimbali ya mazingira ikiwa ni pamoja na Shirika la WWF na Greenpeace walikusanyika nje ya kituo cha maonyesho na mkutano wa mazingira mjini Busan wakitoa wito wa  kupitishwa kwa  mkataba wa plastiki wenye nguvu zaidi ili kukabili uchafuzi wa mazingira.

Wapatanishi kutoka karibu nchi 200 wanakutana kwa faragha kujadili mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki. Ikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya wapatanishi kukubaliana juu ya mpango wa kwanza wa dunia wa kushughulikia taka za plastiki , rasimu mpya iliyotolewa leo ijumaa imeonyesha kuna kutokukubaliana kwa kiwango cha juu.

Lengo la waliohudhuria ni kuandaa makubaliano kufikia Jumapili, na kuhitimisha miaka miwili ya mazungumzo juu ya makubaliano ya kihistoria.

Wanaharakati wa hali ya hewa wakidai hatua thabiti zichukuliwe kudhibiti takataka za plastiki katika mkutano wa UN, huko Busan, Korea Kusini, Novemba 23, 2024.
Wanaharakati wa hali ya hewa wakidai hatua thabiti zichukuliwe kudhibiti takataka za plastiki katika mkutano wa UN, huko Busan, Korea Kusini, Novemba 23, 2024.

Saa 48 tu kabla ya mazungumzo yaliyopangwa kukamilika, makubaliano ya awali yaliyotolewa na mwanadiplomasia aliyekuwa mwenyekiti wa mchakato huo yaliibuka, yakiwa na maono yanayoshindana na kutokuelewana.

Kuna ufafanuzi nane uliotolewa kukabili plastiki pekee lna maono tano ya jinsi ya kukabili tishio la plastiki.

Forum

XS
SM
MD
LG