Wanamgambo wa kiislamu hufanya mara kwa mara mashambulizi katika eneo hilo.
Gari lililokuwa limebeba bidhaa za wanajeshi lilikanyaga bomu hilo la kutegwa ardhini nyakati za asubuhi kwenye umbali wa kilomita 6 kutoka kijiji cha Samira, jeshi limesema katika taarifa.
Ni shambulio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Niger.
Nchi hiyo maskini ya eneo la Sahel inakabiliana na uasi wa wanamgambo wa kiislamu wanaohusishwa na Al-Qaeda na kundi la Islamic State.
Katika eneo la kusini magharibi, wanajeshi wa serikali wanapambana pia na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Niger inasaidiwa na nchi kadhaa za magharibi, zikiwemo Ufaransa na Marekani, ambazo zote zina kambi za kijeshi huko.