Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 25, 2022 Local time: 17:13

Wanaharakati wa Misri wasema ukeketaji umeongezeka


Watu wamekusanyika kuwaangalia wasichana kutoka kabila la Sebei nchini Uganda ambao wamefanyiwa ukeketaji katika Wilaya ya Bukwa.
Wanaharakati wa Misri wana wasi wasi kwamba wanasiasa wa kiislamu huenda wakadumaza juhudi za miaka kadhaa kushawishi dhidi ya ukeketaji wanawake. Mwandishi wetu Elizabeth arrott akiwa Cairo anaripoti kuwa utaratibu huu, na harakati dhidi yake zimeota mizizi nchini Misri.

Kwa wafuasi wa utaratibu huu, ni ishara ya usafi, jamii na imani kubwa ya kidini. Kwa wapinzani, ni manyanyaso ya kimwili ya kumdhalilisha mwanamke.

Ukeketaji wanawake maarufu kama FGM ni utamaduni wa enzi na enzi nchini Misri, huku ukizungumziwa kutendwa na wote wakristo na waislamu.
Ukeketaji Misri
please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:05:25 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Utaratibu huu bado umesambaa, ikikadiriwa kuwa hivi leo asilimia 90 ya wanawake nchini Misri wameathiriwa na FGM.

Misri tangu mwaka 2008 imesema kuwa aina yoyote ya ukeketaji ni uhalifu na wafuatiliaji wa haki wanasema kuwa idadi ya wasichana wanaofanyiwa hivyo imeshuka kwa takriban theluthi moja.

Lakini Nehad Abud Komsan, mkurugenzi wa kituo cha haki za wanawake, anasema kuingia katika mamlakani kwa Muslim Brotherhood na wanasiasa wa kiconservative wa Salafist kunatishia mafanikio yaliyopatikana.

"Wanasema, inawezekana kuna sheria ya kuhalalisha hilo kwa aina fulani, au kusema ni vizuri kwa hifadhi. Wanaharibu miaka kadhaa ya juhudi za kuwalinda wasichana na wanawake nchini misri, bahati mbaya wanatumia dini."

Mahakama zimepinga changamoto za kisheria kwa marufuku iliyowekwa sasa, lakini sekta ya sheria na serikali ya Rais Mohammed Morsi wakiwa katika mivutano, wasi wasi unazidi kuongezeka. Ukiongezea wasi wasi kuna ubashiri kuwa wasalafist wanatarajiwa kufanya vizuri katika uchaguzi wa bunge baadae mwaka huu.

Komsan anasema kazi za mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo na kuheshimu kile kinachofanywa ni kiini katika kubadili mtizamo kuhusu FGM
.
Amewagawa watu wale wanaounga mkonoFGM katika makundi matatu. Wale ambao wanaouna ni sherehe za kijamii na kimila, wale ambao wanaamini itawasaidia wanawake kudhibiti hamu yao ya ngono na wale ambao wanaamini kuwa ni jambo linaloelezewa katika dini.

Anasema kutoa njia mbadala ni rahisi sana kwa makundi mawili ya kwanza. Kwa kutumia njia nyingine ambayo si ya kutisha kama vile ukeketaji wa kienyeji ambao unaashiria kwa msichana kuingia katika hali ya kuwa mwanamke au kukubalika katika jamii, hilo linaweza kufanyika bila ya haya kukata hata sehemu moja ya mwili wa msichana.
Mwanaharakati wa masuala ya siasa Hala Galal anaelezea juhudiza za kijiji kimoja ambacho kimechukua uamuzi wa kupinga ukeketaji.

"Hata mwanamke ambaye alitakiwa kufanya operesheni hiyo mwenyewe, kwa kutumia mkono wake, pia ameapa kuacha kabisa utamaduni huu na kufanya shughuli nyingine kama vile kuandaa tafrija za harusi. Nina maana amebadili kazi yake."

Kwa wale ambao wanadhani ukeketaji utawazuia wanawake kuelezea kuhusu hali yao ya uke, Komsan anadai kwamba kuwapa mawazo mengine ndiyo kunaweza kusaidia zaidi na mwelekeo uwe wa kibinadamu.

Lakini yote haya yanahitaji mapambano mazito kwa wanaharakati wanaopinga ukeketaji, lakini jambo moja la kuangaliwa ni kwamba kuna mafanikio katika nyanja ya sheria na kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa. Wasi wasi wao hivi sasa ni kwamba katika hali ya hewa ya sasa ya kisiasa, njia iliyo mbele yao inaweza kuwa ndefu sana.
XS
SM
MD
LG