Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:51

Wanaharakati wa Mau Mau waruhusiwa kuishitaki Uingereza

Muthoni Wanyeki, msemaji wa umoja wa wanaharakati wa Mau Mau akizungumza na waandishi wa habari
Muthoni Wanyeki, msemaji wa umoja wa wanaharakati wa Mau Mau akizungumza na waandishi wa habari

Baada ya madai hayo kukataliwa mwaka 2011, London baadae ilidai kuwa muda mwingi ulipita kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki.

Mahakama moja nchini Uingereza imesema kwamba wazee watatu raia wa Kenya wanaweza kuendelea na mashtaka yao dhidi ya serikali ya uingereza kwa shutuma za mateso wakati wa uasi wa wa mau mau enzi ya ukoloni.

Wakenya hao watatu ambao hivi sasa wapo katika umri wa miaka ya 70 na 80 wanasema walipigwa na kunyanyaswa kingono na maafisa wa kikoloni wa Uingereza walipokuwa wakijaribu kukandamiza uasi katika miaka ya 1950.

London imejaribu kuzuia mashtaka hayo ikisema jukumu la hatua kwa shutuma hizo zilihamishiwa kwa serikali ya Kenya kufuatia uhuru mwaka 1963.

Baada ya madai hayo kukataliwa mwaka 2011, London baadae ilidai kuwa muda mwingi ulipita kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG