“Mara baada ya kuwasili kazini nikuelekea chooni nalia mpaka pale ninapokuwa tayari kuingia kazini nikijaribu kuondokana na huzuni na kutabasamu mbele ya watu,” amesema Mittelsted ambaye huwezi kutambua kuwa ana majonzi, akijaribu kuzuia hisia zake.
Katika eneo jingine la kufanya malipo, Brandy Kraft anajaribu kutabasamu kwa wateja, lakini siyo rahisi kwa sababu anawajua baadhi ya wale 10 waliouwawa katika shambulizi hilo.
“Kwa hakika inatia wasiwasi kuwa katika jamii ambapo unahisi kuwa uko salama na baadae kila amani hiyo inachukuliwa kutoka kwako kabla hujamaliza kupepesa macho. Wengi kati ya marafiki zangu, wakaribu sana wengine mafariki wa kike tunaoshirikiana katika kikundi cha Scout wameuwawa,’ Kraft amesema.
Mittelsted amesema ilimlazimu kurudi kufanya kazi siku moja baada ya mauaji hayo yaliyotokea shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas.
“Wakati huu ninalazimika kujizuilia kuendelea kufikiria hilo kwa sababu kuna watu wamejeruhiwa na wengine wameuwawa. Mimi siyo mmoja wao kwa hiyo ni lazima nishukuru kwa kuendelea kuwa hai na nisijilaze kitandani na kuanza kufikiria” je ingekuwa vipi,” amesema.