Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 19:00

Wakenya watawala Boston marathon


Wesley Korir ashinda mbio za wanaume, Sharon Cherop aibuka na ushindi upande wa wanawake

Wanariadha wa Kenya walitawala mbio ndefu za Boston marathon Jumatatu kwa kushinda nafasi zote tatu za juu kwa upande wa wanaume na wanawake.

Mwanadada Sharon Cherop alitimuka vikali katika mita 800 za mwisho kumtoka Mkenya mwenzake Jemima Jelagat Sumgong aliyekuwa akienda naye sambamba mbio nzima. Cherop alimaliza katika muda wa saa mbili dakika 31 na sekunde 50 wakati Sumgong aliingia sekunde mbili baadaye. Georgina Rono alishika nafasi ya tatu katika muda wa saa mbili, dakika 33 na sekunde tisa. Firehiwot Dado wa Ethiopia alichukua nafasi ya nne.

Kwa upande wa wanaume Wesley Korir ambaye hakutazamiwa kushinda mbio hizo alimtoka Levy Matebo na kumaliza wa kwanza katika muda wa saa mbili, dakika 12 na sekunde 40 wakati Matebo alimaliza na saa mbili, dakika 13 na sekunde sita. Bernard Kipyego alimaliza wa tatu katika muda wa saa mbili dakika 13 na sekunde 13. Mmarekani Jason Hartman alimaliza wa nne.

XS
SM
MD
LG