Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 19:07

Wakazi wa Las Vegas wajitolea kutoa damu kwa waathirika


Ufyatuaji risasi huko Las Vegas, Nevada.
Ufyatuaji risasi huko Las Vegas, Nevada.

Wakazi huko Las Vegas wanapanga mistari kwa takribani saa nane wakisubiri kuchangia damu kwa waathirika kufuatia ufyatuaji risasi mbaya wa umma katika historia ya Marekani.

Mfyatuaji risasi aliyetambulika kama Stephen Paddock mwenye miaka 64 kutoka mji wa Mesquite katika jimbo la Nevada nchini Marekani alifyatua risasi kwenye umati wa zaidi ya watu 22,000 waliohudhuria tamasha la muziki wa “Country” siku ya Jumapili usiku kabla ya kujiuwa mwenyewe wakati polisi wakimkaribia.

Eneo la tukio Las Vegas, Nevada, Oct. 2, 2017.
Eneo la tukio Las Vegas, Nevada, Oct. 2, 2017.

Paddock alifyatua risasi kutoka kwenye chumba kimoja cha hoteli ya Mandalay Bay Resort and Casino katika dhorofa ya 32 jengo linalopakana na mahala ambako tamasha hilo la muziki lilikuwa likifanyika. Watu 59 waliuwawa na 527 walijeruhiwa.

Sherif wa jimbo la Nevada katika kaunti ya Clark, Joe Lombordo alisema polisi waligundua silaha 16 ndani ya chumba cha mshukiwa, milipuko 18 na maelfu ya risasi zilipatikana nyumbani kwa Paddock huko Mesquite.

Rais Trump (L) na Makamu Rais wakiwa pamoja na wake zao
Rais Trump (L) na Makamu Rais wakiwa pamoja na wake zao

Rais wa Marekani Donald Trump aliongoza kipindi cha kukaa kimya katika eneo la South Lawn huko White House akiuangalia mnara wa Washington kama ishara ya kuwakumbuka waathirika.

XS
SM
MD
LG