Huo ulikuwa mkusanyiko wa pili kwenye bustani ya Wencesias mjini humo, baada ule wa Machi 11, ulioitishwa na chama kipya cha kisiasa cha PRO, kinachoshinikiza kutokomezwa kwa umaskini. Waandamanaji, wazungumzaji pamoja na kiongozi wa chama hicho cha uanaharakati Jindrich Rajchi waliilaumu EU na serikali ya Czech kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu, wakiitaka serikali iliyoundwa na muungano wa vyama vitano kujiuzulu. Chama cha Rajchi hata hivyo hakina kiti hata kimoja bungeni, lakini amedai kuwa chama hicho kiko tayari kuendeleza maandamano hayo .
VOA Direct Packages
Wakazi wa Czech waandamana mjini Prague, kulalamikia ugumu wa maisha.
Maelfu ya waandamanaji Jumapili walikusanyika mji mkuu wa Czech wa Prague, wakilalamikia kuongezeka kwa mfumuko wa bei na hivyo kuitaka serikali kujiuzulu.