Polisi wa Austriali wanalaumu mivutano miongoni mwa jamii za waafrika wahamiaji zimesababisha mapigano mabaya huko Adelaide. Viongozi wa wahamiaji wa kiafrika nchini Australia wameomba juhudi zifanywe kupunguza mizozo na ghasia.
Mkuu wa Jumuiya ya wasudan kusini mwa Australia, amesema anadhani waathirika wa ghasia na wale waliotenda ghasia ni wasudan wenyewe. Mabok Deng Mabok alizungumza na polisi leo Jumanne na kutaka mjadala ufanyike na vyama vingine vya wahamiaji wa Afrika kote nchini Australia.
Wahamiaji wa kiafrika na wakimbizi kutoka kote nchini humo wamekusanyika huko Adelaide kwa ajili ya mashindano ya mwaka ya Miss Africa, na baadae mapigano yalizuka saa sita usiku Jumapili.
Vijana wanne wa kiume walichomwa visu katika mapigano hayo ambayo yalihusisha wanaume 100. Mmoja ya wale waliojeruhiwa amefanyiwa upasuaji hivi leo na bado amelazwa hospitali akiwa na hali mbaya sana.
Wanaume wanne wamekamatwa, wawili kati yao wanaishi magharibi mwa Australia, na watatu anatokea eneo la Victoria.