Mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris anafanya kampeni huko Michigan Jumapili huku mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump akisimama katika majimbo matatu ya mashariki yenye ushindani mkali ikiwa ni siku mbili tu kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani siku ya Jumanne.
Kura za maoni zinaonyesha ushindani mkali wa karibu sana kihistoria na ukusanyaji maoni uliofanywa na New York Times na Siena uliochapishwa siku ya Jumapili umewaonyesha Makamu wa Rais Harris na Rais wa zamani Trump wakiwa sawa katika majimbo saba ambayo huenda yakaamua matokeo ya Jumanne.
Kura nyingine ya maoni ilionyesha Harris akiongoza katika jimbo la Iowa ambalo Trump alishinda kwa urahisi katika chaguzi mbili zilizopita, na hivyo kuongeza uwezekano wa matokeo yasiyotarajiwa, ingawa kura nyingine ilionyesha akiwa nyuma katika jimbo hilo.
Forum