Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:37

Wafanyakazi wa sekta ya madini huko Mali wasitisha mgomo


Wafanyakazi wa sekta ya madini wakiwa kazini.

Wafanyakazi katika sekta ya madini nchini Mali wameakhirisha mgomo wa siku tano baada ya ombi la dakika za mwisho kutoka wizara ya madini nchini Mali, alisema afisa wa umoja wa wafanyakazi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters wafanyakazi wa sekta ya madini walipanga kugoma kupinga kile wanachokielezea kuendewa vibaya umoja wa wafanyakazi ambao wamefukuzwa kazi au kupewa adhabu za kinidhamu.

Mahamadou Konte, mwanachama wa Synacom, kampuni ya ujenzi na uchimbaji madini alisema wizara ya madini imeingilia kati baada ya mazungumzo ya ijumaa kushindikana kati ya wafanyakazi na kutaka mashauriano zaidi yafanyike. Alisema kufuatia hatua ya waziri kuingilia kati wameamua kuakhirisha mgomo wao.

XS
SM
MD
LG