Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:11

Waasi wa Libya wateka mji wa Yafran


Shambulizi la anga la Nato katika eneo la Moammar Gadhafi.
Shambulizi la anga la Nato katika eneo la Moammar Gadhafi.

Mashambulizi ya anga ya Nato yasaidia waasi kuteka mji mwingine.

Waasi wa Libya wanasema wameteka mji wa magharibi wa Yafran kutoka kwa majeshi yanayomtii kiongozi Moammar Gadhaffi baada ya mashambulizi ya anga ya wiki iliyopita kuharibu malengo muhimu ya kijeshi ya serikali na kusaidia majeshi ya upinzani kusonga mbele.

Wapiganaji wa kikabila wa Berber ambao wameunga mkono uasi wa serikali walichukua tena Yafran kiasi cha kilometa 100 kusini magharibi mwa Tripoli jumatatu.

Majeshi yanayomuunga mkono Gadhaffi yalishambulia eneo la milima ya magharibi baada ya watu wa eneo hilo wa kabila la Berber kupambana dhidi ya majeshi ya serikali mwanzoni mwa uasi.

XS
SM
MD
LG