Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 01:26

Viongozi wa Ulaya wakosolewa kwa kukosa matayarisho Afghanistan


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris johnson

Maafisa wa Marekani sio peke yao wanaokabiliwa na lawama kwa kuhesabu vibaya kasi ya mashambulizi ya Taliban.

Viongozi wa Ulaya na washauri wao wa usalama pia wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa maamuzi yasiyo sahihi.

Ukosefu wa matayarisho na jinsi matukio yalivyokwenda haraka nchini Afghanistan, mara tu Rais Joe Biden alipoamua kuondoa majeshi ya Marekani kutoka taifa hilo la Asia ya kati.

Huko Uingereza Waziri Mkuu Boris Johnson na mawaziri wake wa ngazi ya juu wanashutumiwa na wabunge kutoka chama chao na vile vile wanasiasa wa upinzani kwa kushindwa kuwa na mipango ya uokoaji.

Lawama hizi zimeibuka baada ya kuonekana kuwa serikali hizi hazikuwa tayari kabla ya uwezekano wa kuongezeka kwa Taliban wakati wanajeshi wa Marekani na NATO walipokuwa wakiondolewa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG