Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:59
VOA Direct Packages

Viongozi wa mataifa ya Afrika ya kati kufanya kikao cha kiuchumi, Ijumaa Yaounde, Cameroon


Daniel Ona Ondo,mkuu wa kundi la mataifa ya Afrika ya kati, CEMAC akizungumza na wanahabari mjini Douala Cameroon. Dec. 26, 2019.
Daniel Ona Ondo,mkuu wa kundi la mataifa ya Afrika ya kati, CEMAC akizungumza na wanahabari mjini Douala Cameroon. Dec. 26, 2019.

Mawaziri wa uchumi kutoka mataifa ya Afrika ya Kati wanatoa wito wa  uwekezaji kwenye sekta za nishati na kilimo, wakati eneo hilo maskini sana barani Afrika likijitahidi kujikwamua  kutoka kwenye  majanga  ya asili,  mizozo ya silaha  pamoja na athari kutokana na  uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Mawaziri kutoka mataifa 6 wanachama wa CEMAC ambayo ni Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Equatorial Guinea, Gabon na Jamhuri ya Congo, walikutana Alhamisi mjini Yaounde. Rais wa CEMAC Daniel Ona Ondo aliyezaliwa Gabon amesema kwamba uvamizi wa Russia nchini Ukraine ndilo janga la karibuni zaidi la kimataifa kuliathiri eneo hilo.

Kabla ya Russia kumvamia jirani yake Ukraine, mataifa ya mataifa ya Afrika ya kati yalikuwa yanaagiza bidhaa kutoka Russia na Ukraine kwa kiwango cha asilimia 60 kwa bidhaa za mafuta na asilimia 80 kwa upande wa ngano. Julai mwaka jana, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Gabon zilitangaza uhaba mkubwa mafuta, zikilaumu vita vya Russia.

Mawaziri waliohudhuria kikao cha Alhamisi wamesema kwamba watapendekeza mpango wa kuimarisha hali kupitia uwekezaji wa nishati na kilimo wakati wakikutana na wakuu wa nchi Ijumaa. CEMAC linasema kwamba mkutano wa leo wa viongozi wa nchi wanachama utaangazia mageuzi ya kiufundi ili kukabiliana na athari za kiuchumi kutokana na janga la Covid pamoja na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG